BEKI mahiri wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Sol Campbell, amewaonya mashabiki wa England wanaotazamia kwenda kushuhudia fainali za Euro 2012, kuwa wasisafiri vinginevyo �wataishia kurudi katika majeneza�.

Campbell anaamini kwamba kwenda nchi za Ukraine na Poland wakati huu ni kujitaharisha kwa kiasi kikubwa kutokana na nchi hizo kukabiliwa na vurugu pamoja na ubaguzi wa rangi.

Nyota huyo wa zamani wa Tottenham ambaye aliichezea England mechi 73, alisisitiza kwamba Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limechemsha kupeleka michuano mikubwa na yenye sifa kama hiyo katika nchi hizo.

�Bakini nyumbani, tazameni katika televisheni. Msijihatarishe kabisa kwa sababu mtaishia kurudishwa katika majeneza. Nadhani walichemsha (Kupeleka michuano hiyo nchini za Poland na Ukraine), kwa sababu wangewaambia �Kama mnataka tulete michuano hii huku malizeni matatizo hayo�.� Alisema Campbell.

�Wangewaambia �mpaka mmalize matatizo yenu, kamwe hatuwapi michuano hii. Hamstahili michuano hii katika nchi zenu.�

Kauli ya Campbell imekuja wakati ambapo familia za baadhi ya wachezaji weusi wa England kama vile Theo Walcott, Joleon Lescott na Alex Oxlade-Chamberlain, zimepanga kutokwenda huko zikihofia matatizo ya ubaguzi wa rangi.

Baba wa Oxlade-Chamberlain, Mark Chamberlain, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England alisikika akisema: �Kumekuwa na ripoti za matatizo ya ubaguzi wa rangi na vitisho kwa hiyo ni jambo zuri kama nikikaa kando.�

Jana Jumatatu, Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, lilitarajia kuonyesha kipindi kinachohusu mashabiki wa nchi hizo wakionyesha vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa kupiga saluti za kundi la Nazi.

Pia lilitarajia kuonyesha jinsi mashabiki hao wanavyozomea kwa sauti za nyani dhidi ya wachezaji weusi na huku pia wakionyesha jinsi wanafunzi wenye asili za Asia wakishambuliwa katika Mtaa wa Metalist jijini Kharkiv.

Mji huo ni wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine na utaandaa mechi tatu za makundi za England.

Popular posts from this blog

MAMBO 6 YA KUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO

Mwanajeshi Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

MATAJIRI WATANO WANAOONGOZA TANZANIA