Posts

BENKI YA NBC WATOA ZAWADI ZA X-MAS NA MWAKA MPYA

Image
by David Mathias on December 26, 2012                     Baadhi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA, Sinza jijini Dar es Salaam wakionyesha baadhi ya vitu walivyopewa kama  msaada na wafanyakazi wa Benki ya NBC kituoni hapo juzi ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya. .                      Meneja Mwandamizi Idara ya Utendaji wa Benki ya NBC, Salim Rupia (kulia) akikabidhi msaada vyakula na vitu vingine vilivyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, ndugu Ally Saidi kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi  ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu za Christmas na mwaka mpya.         ...

RAIS JK ASHEREHEKEA KRISMAS MBUGANI SERENGETI

Image
by David Mathias on December 25, 2012                     Mabingwa wa Kombe la Ujirani Timu ya hoteli ya Seronera wakifurahia ushindi baada ya kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge  katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo. Hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao. (PICHA NA IKULU)                        Nahodha wa hoteli ya Seronera Jamali Kitonga akifurahia baada ya kukabidhiwa kombe la Ujirani mwema na Rais Jakaya Kikwetebaada ya timu yake kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara...

JK AWAFUNGULIA MBWA MWITU 15 MKOANI MARA

Image
by David Mathias on December 25, 2012              Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. (PICHA NA IKULU)                    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, ...

LAWRENCE MAFURU RESIGNATION

Image
by David Mathias on December 25, 2012                                                                            I have today 24th December 2012 submitted my formal resignation as Managing Director of NBC t o the Chairman of the Board of Directors of NBC to pursue other opportunities outside NBC. As I had mentioned in my letter to the Chairman, this has not been an easy decision but as career person, there are times in our career life we have to make difficult decisions. The decision to relinquish my position is completely in line with my career objectives. After 4 years of a very pro...

Mh. Lowassa ashiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismas Visiwani Zanzibar leo

Image
by David Mathias on December 25, 2012 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar. Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo leo.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

Meya Jerry Silaa ashiriki katika kampeni ya Usafi Katika Kata ya Gongo la Mboto.

Image
  Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto, Jerry Silaa akiwa na baadhi ya  wakazi wa Kata hiyo wakifanya kazi ya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu. Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto,Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya  wakazi wa Kata hiyo wakati wa kufanya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu

Mechi kati ya Taifa Stars na Chipolopolo ya Zambia yaingiza Tsh. Mil 109/-.

Image
  Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000. Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000. Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138...